Quantcast
Channel: TANZANIA ONE
Viewing all 110 articles
Browse latest View live

Utata mpya mtoto wa Diamond!

$
0
0
Diamond-Platnumz-na-Zari
Staa wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,  akiwa katika pozi na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
MUSA MATEJA
Utata mpya umeibuka wakati mama kijacho wa staa wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,  akitarajiwa kujifungua muda wowote kutoka sasa, ishu ni juu ya uraia wa mtoto atakayezaliwa.
TUJIUNGE NA MTU WA NDANI
Habari kutoka kwa mtu wa ndani wa familia hiyo zilidai kwamba, utata umezidi kuigubika familia hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ndugu wa pande zote kuendelea kuvutana juu ya Zari ajifungulie nchi gani kati ya Tanzania, Uganda na Afrika Kusini ‘Sauz’.
DIAMONDZARI.jpg
Utata huo umevuja wakati paparazi wetu akiwa katika mishemishe za kutaka kujua Zari alipo kwa sasa na atajifungulia katika hospitali ipi ndipo alipopenyezewa ‘ubuyu’ kwamba hadi sasa kuna utata mkubwa katika familia hiyo.
MABISHANO YA URAIA
Chanzo kilimweleza mwanahabari wetu kuwa, kikubwa ni mabishano ya uraia na sehemu sahihi ya kujifungulia mtoto huyo.
Kilidai kwamba, suala hilo limekuja kufuatia ndugu wa Zari kutaka ajifungulie Sauz jambo ambalo Diamond na familia yake wamekuwa wakilipinga vikali.
ZARINADIAMOND4.jpg
ZARI NJIA PANDA
Ilisemekana kwamba, kwa upande wake Zari amekuwa njia panda kutokana na shinikizo hilo huku mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ naye akisisitiza kuwa lazima Zari ajifungulie Bongo ili amuhudumie mkwe wake huyo.
“Yaani ndugu wa Zari wanampa Diamond wakati mgumu sana kutokana na kuendelea kung’ang’ania Zari akajifungulie kwao (Sauz ambako kuna ndugu wengi) wakati furaha ya Diamond ni kuona mtoto akizaliwa Bongo.
DIAMOND ACHACHAMAA
“Unaambiwa Diamond amechachamaa vibaya, alipoona hawezi kutumia nguvu ikabidi atumie ushawishi kwa ndugu wa Zari ili wakubali ajifungulie Bongo lakini wale ndugu wanasema wako tayari kumtumia hata ndege kwa sababu yupo Bongo, arudi Sauz ambako kuna daktari wao wa familia.
HUYU HAPA DIAMOND
Paparazi wetu baada ya kunyaka utata huo alimtafuta laivu Diamond kwa kujiridhisha zaidi juu ya hilo ambapo baada ya kumpata alifunguka kwamba, kipindi hiki kuna mambo kibao yanaibuka kila kukicha jambo linalomshangaza.
zari
Alisema kuwa utata huo alishamalizana nao ndiyo maana hadi muda huu Zari yupo Dar kwa ajili ya kujifungua.
“Ninachoweza kusema kwenye maisha ya kawaida huwezi kuwazuia watu kuongea jambo wanaloliwaza wao.
“Hayo mambo ya utata nimeshayamaliza ndiyo maana kwa sasa Zari yupo White House (nyumbani kwa Diamond, Tegeta-Madale jijini Dar) akisubiria saa ya kujifungua.
“Kwangu namuomba Mungu ajifungue salama maana mtoto ni miongoni mwa vitu nilivyotamani kitambo,” alisema Diamond huku akiwashukuru Watanzania wote wanaoendelea kumuunga mkono kwenye muziki wake.

Hii ni tweet ya Martin Kadinda baada ya Wema Sepetu kushindwa viti maalumu Singida

$
0
0
Wema Sepetu bahati imekuwa sio yake, baada ya kushindwa katika uchaguzi wa viti maalumu katika mkoa wa Singida.
wemaa-na-kadinda
Meneja wa Wema sepetu ameandika kuhusu kushindwa kwa Wema Sepetu katika uchaguzi huo…Katika Mtandao wa Twitter Martin Kadinda ameandika “Haikuwa vile tulivyotarajia… Hongera Aysharose Mattembe”.

Diamond Platnumz ameshinda tuzo zingine mbili

$
0
0
Msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz ameshinda tuzo zingine kubwa Afrika, kupitia kurasa yake ya instagram ametufahamisha kuhusu ushindi huu na tuzo.
  Thanks alot to my all Fans around the World, for your unconditional love and Support that you been Giving me… i can’t even explain how grateful i am… two awards on NollyWood & African People Choice Awards @Africannafca
FAVOURITE SONG OF THE YEAR (Nana)
FAVOURITE ARTIST OF THE YEAR
thanks alot @Africannafca 🙏
(Naomba nitumie Muda huu kuwashkuru Mashabiki zangu wote kwa Mapenzi na Sapoti yenu ya Dhati mnayoendelea kunipa…ningependa niwataarifu kuwa kijana wenu mmeniwezesha kushinda tunzo mbili ambazo ni MSANII ANAEPENDWA AFRICA na NYIMBO INAYOPENDWA AFRICA (#NaNa ) kwenye Tunzo za NollyWood & African people Choice Awards @Africannafca zitazotolewa tareh 12 /09 /2015 🙏
 ” Hongera Diamond Platnumz.
winners
winner 2

Nuh Mziwanda amuomba penzi Wema!

$
0
0

Musa Mateja

YELEUWIII! Katika hali ya kushangaza, sauti ya mpenzi wa staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ inayosikika akimtongoza Wema Sepetu imemfikia Shilole na kusababisha azimie, Ijumaa Wikienda linakupa ‘ubuyu’ kamili.

BETHIDEI YA SHAMSA Tukio hilo lililozua mtafaruku lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kulipokuwa na pati ya bethidei ya mwigizaji Shamsa Ford.

TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kilishuhudia tukio hilo mwanzo-mwisho, saa chache baada ya kumalizika kwa shughuli ya kulishana keki, waalikwa walishangaa kumuona Shilole akiishiwa nguvu na kudondoka baada ya kusikiliza ujumbe wa sauti aliotumiwa kwenye simu.“We acha tu. Ilikuwa balaa. Watu tulikuwa katika shamrashamra ya kulishana keki, ghafla tukashangaa mwenzetu anaishiwa nguvu na kuanguka,” kilieleza chanzo.

nuhumziwanda.pngStaa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,  akiwa na mpenzi wake wa sasa Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.

UJUMBE ULISEMAJE? Chanzo hicho kilitiririka kuwa, ujumbe huo wa sauti ulisikika Nuh akimuimbisha Wema kwa maneno ya kimahaba. “Nuh kajipambanua ileile. Kaimbisha mistari yote ya kimahaba, utafikiri alikaririshwa. Alijitahidi kushusha vesi tamu ili  kumuingiza Wema kwenye himaya yake. Huwezi amini jamaa alizidisha mbwembwe kiasi cha kumwambia amkubalie kwani hamtaki Shilole tena. WEMA AMTOSA “Wema amesikika akikataa, akamwambia hawezi kuwa naye kwani ni shemeji yake na anamheshimu Shishi,” kilisema chanzo hicho.

wema 2Wema Sepetu.

SHILOLE AMFUATA NUH Chanzo hicho kilieleza kuwa, baada ya kuusikiliza ujumbe huo, Shilole alimfuata Nuh kwa ajili ya kumsikilizisha lakini Nuh alijibu ‘mbovu’ ndipo Shilole alipomuomba ufunguo wa gari waliyokwenda nayo, akarudi alipokuwa amekaa awali.

APOTEZA ‘NETIWEKI’ “Aliporudi alipokuwa amekaa, Shilole alijikuta akiishiwa nguvu na kuzimia ambapo Aunt Ezekiel na kina JB (Jacob Stephen) walipofanya kazi ya ziada kumpepea, huku wengine wakihangaika kummwagia maji kunusuru afya yake. “Walifanikiwa kumpandisha kwenye gari lake. Joto lilikuwa kubwa kufuatia hali hiyo maana kila mtu alishindwa kuelewa kilichotokea, hivyo Shilole, baada ya kuzinduka aliulizwa kilichomfanya azime ambapo aliwasikilizisha sauti hiyo kila mmoja akabaki ameduwaa,” kilieleza chanzo.

WemaSepetu.jpgAUNT AOKOA JAHAZI Ilielezwa kuwa, mwigizaji Aunt Ezekiel ndiye aliyeokoa jahazi kwa kulazimika kuendesha gari la Shilole na kumpeleka nyumbani huku Nuh akipandishwa kwenye gari la JB kumpeleka kwa ndugu zake.

MSIKIE SHILOLE Paparazi wetu, baada ya kupenyezewa ubuyu huo, alimtafuta Shilole ili kupata habari kamili ambapo alikiri kupokea ujumbe huo wa sauti huku akiainisha kuwa umemkera kwani kuna maneno yanasikika akimponda yeye. “Inaniuma sana, Nuh kuendelea kunidhalilisha kiasi hicho wakati ni mwanaume ambaye ninamheshimu, tunakoelekea uzalendo utanishinda.

“Nilipousikiliza ujumbe ule kwa mara ya kwanza sikuamini nilichokisikia. Pamoja na Wema kuonesha wazi msimamo wa kumkataa Nuh ila mimi naona kama fedheha kubwa kwangu kwani ninamheshimu sana. “Watu wananiona mimi mkorofi lakini kama ningekuwa napenda kuweka kila jambo wazi, hakuna mtu angeendelea kunifikiria vibaya.“Siwezi tena kuendelea kuumiza moyo wangu kila kukicha,” alisema Shilole ambaye anatumikia kifungo cha Basata kwa kutojishughulisha na sanaa kwa takriban mwaka mmoja kwa kosa la kucheza nusu utupu jukwaani.

HATIMAYE NAY NA SHAMSA WAKIRI KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI

IDD AZAN AITEKA KINONDONI

$
0
0
2
Idd Azan (katikati), akikatiza Mitaa ya Mkwajuni wakati akielekea kwenye mkutano wake wa kampeni  uliofanyika katika Kata ya Hananasifu, jana jioni.
3
Azan akiteta jambo na Hassan Dalali, mjumbe wa CCM, Kata ya Hananasifu.
45
Hassan Dalali akimkaribisha Azan kwenye kikao cha kampeni muda mfupi baada ya kuwasili mahali hapo.
6
Kikundi cha ‘kudansi’ kikitoa burudani mahali hapo.
7
Azan akinadi sera zake jukwaani  kwa wakazi wa Kata ya Hananasifu, Kinondoni jijini Dar es Salaam, jana jioni.
89,
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan (katikati), akiwa amempakata mtoto aliyejitokeza na wazazi wake kusikiliza sera.
10
Mmoja wa wazee wa Kata ya Hananasifu akizungumza jambo na Azan baada ya kukutana naye njiani alipokuwa akielekea kwenye mkutano.
MGOMBEA wa kiti cha ubunge Jimbo la Kinondoni  kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Idd Azan jana aliwateka baadhi ya wakazi wa jimbo hilo waishio katika kata ya Hananasifu baada ya kukatiza kwa miguu wakati wa jioni alipokuwa akienda kwenye mkutano wa kampeni na baadhi ya wakazi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi na kuandamana naye hadi mahali mkutano ulipokuwa ukifanyikia.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:30 jioni ambapo Azan aliamua kutembea kwa miguu akitokea makao makuu ya ofisi za chama hicho zilizopo Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

HIVI NDIVYO TASWA ILIVYOMUAGA RAIS KIKWETE NDANI YA UKUMBI WA MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM

DANSA WA DIAMOND AIBEBA TIMU YA MPIRA MTAANI KWAO

$
0
0
 Mcheza shoo wa Diamond (wa tatu kutoka kulia nyuma), Dumy Utamu akiwa kwenye pozi la pamoja na vijana wanaochezea timu ya mtaani kwao inayokwenda kwa jina la Young Boyz.



ZIZZOU FASHION YAWAPA VIFAA VYA MICHEZO CHANGANYIKENI RANGERS

$
0
0
Mkurugenzi wa Duka la Zizzou Fashion, Athumani Tippo (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo kocha wa timu ya Changanyikeni Rangers, Steven Nyenge ndani ya duka hilo lililopo maeneo ya Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam.

DUKAla vifaa vya michezo la Zizzou Fashion mapema leo lilijitolea kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya soka ya Changanyikeni Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi Zizzou Fashion, Athumani Tippo alisema kwamba, amelazimika kutoa mchango wake kwa timu hiyo kutokana na kuonyesha juhudi, uwezo na kujituma kwa wachezaji wa timu hiyo kwa muda mfupi tangu ilipoanzishwa.

“Niameamua kutoa mchango wangu wa vifaa vya michezo kwa timu hiyo kwani imenishawishi baada ya kuifuatilia kwa muda sasa ambapo nimeziona juhudi za kocha wao, Steven Nyenge na wachezaji wote kwa ujumla wanavyojituma kuhakikisha wanapanda daraja,” alisema Tippo.
Tippo akiwa katika pozi na kocha wa timu ya Changanyikeni Rangers (katikati), na Kocha wa timu ya watoto ya Boko Beach Veterani, Maswanywa
 MOSHI VETERANI YAWACHAKAZA BOKO

Kikosi cha timu ya Boko Beach Veterani kikiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya mchezo huo kuanza.
 TIMUya wakongwe ya Moshi Veterani Wikiendi iliyopita iliitembezea kichapo Boko Beach Veterani kwa bao 1-0 kwenye mechi ya kudumisha urafiki baina ya timu hizo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Boko jijini Dar es Salaam.
Nahodha  Moshi Veterani, Jafari Kiango (kushoto), akimkabidhi mchezaji wa timu ya Boko, Godfrey Malekano ‘Messi’,  zawadi ya Mchezaji Bora wa Mwezi kwa niaba ya Zizzou Fashion, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

TASWIRA KATIKA PICHA ZA MAPOKEZI YA DIAMOND PLATNUMZ DAR ES SALAAM

Article 0

$
0
0
Baadhi ya wachezaji wa Simba SC, wakishangilia goli lao baada ya kuichapa Mbeya City.

SIMBA Sports Club ya jijini Dar es Salaam, jana imevunja mwiko wa kufungwa na kutoa droo na timu ya Mbeya City baada ya kuwafunga goli moja kwa sifuri katika dimba la Sokoine, ushindi ambao ni historia kwao kutokana na kuteswa na wanakomakumwanya hao kwa mda wa misimu miwili iliyopita.

Histori ya wagonga nyundo  imevunjwa na  Simba kwa goli moja tu maridadi lililowekwa nyavuni na Mganda wa timu hiyo Juuko Murushidi dakika ya pili ya mchezo, goli ambalo katika ligi kuu msmu huu litakuwa la  mapema zaidi katika uwanja huu ukiachia mbal goli la Atupele Green wa Ndanda FC,  liliofungwa dakika ya 3.

Kikosi cha Simba SC, na Mbeya City kikipambana kabla ya Juuko kupachika bao.
Wachezaji wa Simba SC, Mussa Hassani Mgosi na Juuko Murushidi wakishangilia baada ya kuifunga Mbeya City.

Staili ya ushangiliaji ya ina yake iliyoonyeshwa na wachezaji wa Simba.
..wakishangilia kwa pamoja.
Mabosi wa timu ya Simba wakifurahia jambo uwanjani hapo.
Mmoja wa mashabiki wa  Mbeya City akiwa amebebwa kwenye machela baada ya kupoteza fahamu kwenye mchezo huo.



KAMPUNI YA AIRTEL TANZANIA KUUNDA MUUNDO MPYA WA UTENDAJI WA KUBORESHA HUDUMA ZAKE!

$
0
0

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano akifafanua jambo.





Kampuni ya Simu za mkononi nchini Airtel Tanzania, leo imetangaza mkakati wake wa kuboresha muundo katika nafasi zote za utendaji kuwa bora zaidi na kuweka idadi sahihi ili viwango vya kiutendaji kuimarika na hatimae dhamira yake ya pkibiashara ya kutoa huduma na bidhaa bora za kimawasiliano nchini Tanzania kufikiwa.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano alisema “ Mkakati huu wa kuboresha upya mfumo wa utendaji wa kampuni yetu ni sambamba kabisa na mfumo wetu wa maboresho uliowekwa na kampuni yetu ambao tunaamini baada ya muda mfupi utakuwa na mafanikio makubwa kwa wadau wote wakiwemo wafanyakazi na wateja wetu tunaowahudumia”
Singano akifafanua alisema “Maboresha haya tunayofanya yatawahusisha takribani wafanyakazi 55 kwa nafasi zao za utendandaji kutokuwepo au kuhamishiwa kwa wadau watakao toa huduma kwa kampuni yetu, mfumo ujulikanao kama “outsource model”, watoa huduma tutakaowapa jukumu la kusimamia baadhi ya huduma zetu”

Airtel tangu kuanza kwa mkakati huu wa maboresho yake ya kiutendaji kwaajili ya kutimiza malengo ya kibiashara imejizatiti kwa kuweka miundombinu madhubuti kwa kuingia mikataba ya kiutendaji.

“Vilevile kama njia ya kushirikiana na wale watakao guswa na zoezi hili la marekebisho ya mfumo huu kipindi hiki cha mpito, Airtel tayari imeingia mkataba na kampuni inayohusiana na huduma za rasilimaliwatu ili kutoa mafunzo na ushauri wa kutosha ya jinsi ya kutafuta na kuzipokea nafasi zingine zinazojitokeza, Malipo ya huduma hii kwa wote watakaohitaji yamegaramiwa na Airtel” alimaliza kwa kusema Bi, Singano .

HII NDIYO KAULI YA KOCHA MPYA MBEYA CITY MUDA MFUPI BAADA YA KUKABIDHIWA KUIONGOZA TIMU HIYO!

$
0
0
Kocha mpya wa Mbeya City FC, Kinah Phiri (katikati), akizuingumza jambo muda mfupi baada ya kukabidhiwa kuiongoza timu hiyo.
“Nimefurahi kujiunga na timu hii, ni moja ya timu nzuri na kubwa kwenye soka la Tanzania, ila naomba watu watambue kuwa kuijenga City si jukumu langu peke yangu, ushirikiano kutoka kwa uongozi wa jiji, viongozi wa klabu, bodi pamoja na mashabiki naamini utafanikisha kazi yangu na kutufanya sote kufikia malengo, nimekuja katikati ya msimu lengo langu kwanza ni kuhakikisha timu inabaki kwenye ligi, huo utakuwa mwanzo wa ujenzi imara kwa ajili ya msimu mpya”

Kauli ya Kocha mkuu mpya wa City Kinnah Phiri akizungumza mbele ya wana habari mara baada ya kukamilisha zoezi la kutia saini kandarasi yake ya miaka mitatu kuliongoza benchi la ufundi mapema leo kwenye ofisi ya Meya wa jiji la Mbeya.

DIAMOND AINEEMESHA UPYA FAMILIA YAKE!

$
0
0

DIAMOND AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MALIKIA WAKE TIFFAH NA MAMA TIFFAH ZARI THE BOSS LADY.

FAMILIA ya mkali wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ imelamba mamilioni ya shilingi kufuatia mkataba walioingia hivi majuzi na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom, Risasi Mchanganyiko lina ripoti kamili.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ya kampuni hiyo yenye mtandao mkubwa zaidi wa simu nchini, Diamond na familia yake inayowahusisha mama yake mzazi, mzazi mwenzake Zarinah Hassan na mtoto wao Tiffah, wamepewa kiasi cha shilingi milioni 700.“Mimi nipo hapa, mkataba umefanywa kwa usiri mkubwa na unajua haya mambo yanakuwaga kisheria zaidi, lakini dogo (Diamond) kalamba siyo chini ya milioni 700, nadhani ndiyo msanii wa kwanza Bongo kupata mkwanja wa maana kwenye haya matangazo ya biashara,” kilisema chanzo hicho.

Wakati chanzo hicho kikitoa madai hayo, katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kiasi cha fedha kinachotajwa kutolewa katika mkataba huo ni kiasi cha dola 650,000.
Gazeti hili lilimtafuta Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu ili azungumzie madai hayo ikiwemo kiasi halisi ambacho Diamond alipewa.

“Ni kweli kuwa ni jambo jema kama wasanii wachanga na wengine wakijua kiasi halisi cha fedha ambacho Diamond amepewa, ila suala hili lipo kisheria, nitakuwa nimevunja sheria endapo nitasema, kifupi ni kwamba amesaini mkataba mnono na kama Vodacom, tutaendelea kuwasapoti wasanii wetu wa ndani na maisha yao yataendelea kuwa murua.
“Tunachoomba ni kwa wasanii wetu kujituma zaidi na kuwa kioo cha jamii kwa kuwawakilisha Watanzania kwa uweledi,” alisema.

Alisema Vodacom imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Diamond, lakini milango ipo wazi kwake kuweza kusaini upya baada ya huu kumalizika. Aidha, alisema msanii huyo ndiye pekee aliyesainishwa na kampuni yao, lakini Aprili mwaka huu, ambao ni mwezi wa kuanza kwa bajeti yao mpya, wanategemea kuwasainisha wasanii zaidi wa Bongo Fleva.

Kwa upande wake, mmoja wa mameneja wa Diamond, Babu Tale, alikiri msanii wake kupata mkataba mnono kuliko aliowahi kupata msanii yeyote kabla, lakini hata hivyo hana mamlaka ya kutaja kiasi, kwani ni suala binafsi la Diamond.

“Kwanza nikusaidie, hakuna kampuni ya ndani hivi sasa inayoruhusiwa kutoa malipo kwa dola, fedha zote zinatolewa kwa shilingi, lakini kwamba ni kiasi gani kwa kweli siwezi kusema, ila mkataba wake ni mnono kuliko msanii yeyote Bongo kwa sasa.”

Juhudi za kumtafuta mkali huyo anayetamba barani Afrika kwa sasa zilishindikana kwani hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, taarifa zilisema alikuwa Afrika Kusini
Mtoto wa Diamond, Latiffah Nasbu ‘Tiffah’

SOMA BARUA YA OMMY DIMPOZ UONE JINSI ALIVYOMTUKANA WAZIWAZI NAY WA MITEGO,AMBADILISHA JINA AMUITA DADA NEEMA!

$
0
0

Ommy Dimpoz
"Barua ya wazi kwa Neema wa Mitego kwanza pole kwa Malezi ya Watoto ambao mama zao wamekukimbia, hakuna Mwanamke ambae anaweza kuishi na mwanaume mwenye tabia za kike kama zako ?? inatakiwa ujiulize una tatizo gani maana km umaarufu mavi unao,nyumba unayo,magari unayo na hivyo ndo vitu dada zetu wanapenda lakini kwanini wanakukimbia pili kila nikiwaangalia watoto naona kabisa hamjafanana kuna umuhimu wa DNA Da Neema trust me. Vitu navyokula mimi wewe utaishia kuviona kwenye TV maana kuvipata mpaka uwe Unapanda sana Ndege sasa mimi najaza passport ya Tatu wakati wewe hata kurasa 4 za passport yako ya kwanza hujamaliza ??

Nay wa Mitego
Sasa wewe ushazoea wanawake zako wa jumuiya basi unataka kila mtu apost demu wake. Nimekujibu ili nikusaidie promo ya nyimbo yako Atleast upige na Vishoo baba ???? Sema nakuomba usirushe ngumi tu maana nakujua Mzee wa Kupanic Maana katika hao mabebi mama wako kuna mmoja nilishapitaga nae Uliza vizuri atakwambia kama jogoo anawika au vipi".??

UBALOZI WA TUNDAMAN KUIVA,WASANII 12 KUKINUKISHA MWEMBE YANGA MACHI 5 KWENYE TAMASHA LA AMSHA MAMA FESTIVAL

$
0
0
Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo.

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la ‘Amsha Mama Tanzania’ linalotarajiwa kufanyika Machi 5 katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke jijini Dar es Salaam .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy record yenye makao Mkuu yake nchini Kenya ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo Joe mama wa Tanzania kujiinua kiuchumi .

“ Akina mama mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili mahususi kwenu kwa kuwa mtapata fursa mbalimbali na mtaweza kupata mambo mbalimbali ikiwemo elimu” .Alisema Kariuki.

Kwa upande wake balozi wa Amsha Mama nchini Khalid Ramadhani (Tundaman), amewaomba wakinamama wachangamkie fursa kwani watajifunza mambo mengi

“Nawaomba Mama zangu mjitokeze kwa wingi kwani tumepata bahati ya pekee ya kupendelewa kuletewa tamasha nchini kwani ni adimu kutokea,” .alisema Tundaman.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika pia katika uwanja wa Ranchi ya Kedong uliopo jiji la Naivasha nchini Kenya marchi 25-27 huku likitarajia kukutanisha akinamama kutoka nchi zote za Afrika .

Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii kama vile Juma Kassim ‘’Juma Nature’’, Khadija Kopa, Roma Mkatoliki, Young Killer, Msagasumu, Man fungo,Sharo mwamba,Q-Chief,Mr Blue,Snura,Tundaman,na Ally Choki.

Tamasha la Amsha Mama linatarajiwa kukutanisha akinamama mbalimbali kwa lengo la kujifunza kuhusu kujikwamua kiuchumi kwani wao ndio chachu ya mafanikio.

Alisema wamejipanga kuwapa radha tofauti watoto wa temeke na majirani zake ,hasa kwa akina mama kupata fursa ya kujielewa na kujitambua hasa katika kuendeleza familia zao.

LIGI YA NAY WA MITEGO,OMMY DIMPOZ YAFIKIA HATUA MBAYA!

$
0
0

Nay wa Mitego
NGANGALI wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na Omar Faraj Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ wamefika pabaya baada kutukanana mitandaoni.

Ugomvi wa wawili hao uliibuka mapema wiki hii mara baada ya Nay kuachia wimbo wake mpya redioni uitwao Shika Adabu Yako ambao amewachana mastaa wengi wa Bongo Muvi sambamba na Ommy Dimpoz aliyemwambia ana shaka kuwa ana tatizo la kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa.

Baada ya wimbo huo kutoka na kumkasirisha Dimpoz ambaye aliibuka na kujibu mashambulizi mazito mtandaoni, chanzo kimeeleza kuwa wawili hao sasa hivi wanatafutana mtaani ili kuoneshana ubabe laivu.
Ommy DIMPOZ

“Yaani hii vita yao sasa imefika pabaya, watakapokutana tu wawili hawa lazima pachimbike maana kila mmoja anamuwinda mwenzake kwa wakati tofauti,” kilisema chanzo chetu.

Alipotafutwa Nay wa Mitego kuhusiana na suala hilo alisema yeye alitegemea wimbo huo utawakera wengi lakini ndiyo ukweli hivyo yupo tayari kwa lolote na yeye hana mpango wa kumsaka Ommy.
“Sina habari naye huyo kama meseji imemfikia, akae kimya,” alisema Nay.

Kwa upande wake Dimpoz naye hakutaka kukiri kuwa anamsaka Nay lakini akasema amekasirishwa sana na kitendo cha Nay kumuimba vibaya wakati kama ni mpenzi yeye anaye na anamridhisha.

“Yule wewe muache tu. Ameniboa sana. Mimi kweli niwe jogoo hapandi mtungi kweli? Aache hizo, nina demu wangu na anajua nini huwa nampatia,” alisema Dimpoz huku akimtumia mwandishi wetu picha ya mpenzi wake pasipo kumtaja jina.
30SHARES

PENZI LA MBUNGE LAMTESA JOHARI!

$
0
0
Muigizaji wa Bongo Muvi Blandina Chagula 'Johari',
 MUIGIZAJI mkongwe wa filamu Bongo, Blandina Chagula anayefahamika kisanii kama Johari, anadaiwa kuwewesekea penzi la mbunge mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina linahifadhiwa) ambaye alifunga ndoa miezi michache iliyopita.

Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kimeliambia gazeti hili kuwa Johari alikasirishwa na kushangazwa na hatua ya msanii mwenzake kuolewa na mbunge huyo, ilihali akijua kuwa yeye aliwahi kuishi naye kimapenzi, ingawa alikataa kuolewa naye kwa kile alichosema ‘hajatulia’.

“Johari anaweweseka kweli jamani, yaani kinachomuuma huyo mke wa mheshimiwa ni yeye ndiye aliyemkutanisha na anajua kila kitu, lakini anashangaa hata ilivyokuwa hadi akakubali kuolewa naye, yaani ni kama mtu aliyeumia sana,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake ili kulinda ushoga wao.

Baada ya kunasa ushahidi unaothibitisha Johari akimzungumzia mbunge huyo kuonesha anaweweseka, gazeti hili lilimtafuta Johari na kumwuliza kuhusu tuhuma hizo, lakini msanii huyo aliruka kimanga, akidai hajawahi kuweweseka kwa penzi la mbunge huyo na wala hajawahi kuwazungumzia.

NAY: NAHISI KUUAWA MUDA WOWOTE!

$
0
0
Picha ya Nay wa Mitego iliyoharibiwa na baadhi ya wapinzani wake kwa lengo la kumchafulia jina.
Nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.

Hali ni tete! Siku chache baada ya nyota wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuwasiliba wasanii wenzake kwenye wimbo wake mpya wa Shika Adabu Yako, ameibuka akidaiwa kujisalimisha polisi kufuatia kutishiwa kuuawa na watu asiowafahamu.

CHANZO CHAWEKA WAZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya kuachia wimbo huo, jioni yake tu, Nay alipigiwa simu na watu asiowafahamu wakimtaka aupotezee wimbo huo kabla haujamgharimu maisha kwa njia yoyote ile.

APUUZA, ATUMIWA MESEJI
Chanzo kilidai kuwa, Nay alipuuzia simu hizo lakini alishangaa ilipofika asubuhi siku iliyofuata, alikuta ujumbe wa maneno (SMS) kwenye simu yake ukiwa na maneno makali na ya kuendelea kumtishia kifo.

Picha iliyotengenezwa kumdhalilisha Ney wa Mitego.

INSTAGRAM NI ZAIDI
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, Nay, akiwa anafikiria namna ya kukabiliana na vitisho hivyo, aliingia kwenye akaunti yake ya Instagram ‘direct’ (moja kwa moja) na ‘hamadi’ akakutana na ujumbe ukiwa na vitisho vya kumuua.

“Jamaa hana raha hata kidogo, amekutana na meseji na simu alizopigiwa. Ameamua kuzima simu zake zote. kilisema chanzo hicho.“Kwa sasa anajiandaa kwenda mkoani Lindi kuna shoo hivyo tunapata hadi wasiwasi kama jamaa ataweza kweli kufanya kazi inavyotakiwa,” Chanzo.

KWENDA POLISI
Imezidi kudaiwa kwamba, baadhi ya watu wake wa karibu na mama yake mzazi, walimshauri aende akaripoti Kituo cha Polisi Kimara (jirani na nyumbani kwake) kwa vile anaweza kupata matatizo makubwa.

MAMA YAKE ANALIA TU
“Mbaya zaidi, mama yake naye, amepaniki kiasi kwamba analia tu. Inabidi sisi ndiyo tumpe moyo maana anafikiria hatima ya mwanaye kwani kila anapokwenda akikutana na watu wanamlalamikia juu ya wimbo huo,” kilisema chanzo hicho.

Kamanda Simon Sirro.

WIKIENDA LAMSAKA
Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Nay kutaka kujiridhisha kuhusu madai hayo lakini hakuwa hewani. Ilibidi kumtafuta mtu wa karibu yake na ndipo alipopatikana.

Naye alikiri kutishiwa kuuawa. Alisema hatua ya awali alichukua uamuzi wa kwenda Kituo cha Polisi Kimara, Dar lakini hakufunguliwa faili la kesi kwa maelezo kuwa, usiku huo askari wasingeweza kufanya hivyo badala yake walimtaka arudi kesho yake.

HUYU HAPA NAY
“Hapa nilipo nimechanganyikiwa. Kwa hali ilivyo nimeona bora niende polisi maana najua nitauawa wakati wowote. Nilikwenda Polisi Kimara lakini sikufanikiwa, sasa najiongeza, nitakwenda Kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (kwa Kamanda Simon Sirro).

Wikienda: “Nimesikia unakwenda Lindi kwenye shoo, sasa huko Polisi Kanda Maalum umeshakwenda au utakwenda ukirudi?”

Nay: “Kwanza nilikwenda polisi pale Kimara, wakashindwa kufungua faili. Waliniambia niende asubuhi lakini nimeshindwa kwa kuwa nimeondoka Dar na hapa nipo Lindi.

“Ila kuna ujumbe nimeukuta Insta (Instagram) ni mbaya sana. Nimepanga nikirudi nienda Kanda Maalum, lakini kuna wenzangu niliokuja nao hapa Lindi wamenishauri niende Kituo cha Polisi Kikuu cha hapahapa nikaripoti.”

TIMU WEMA WAMFANYA VIBAYA
Wakati huohuo, wadau wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (Team Wema), wanadaiwa kuchukua picha ya mrembo huyo akiwa kwenye gari na kuipachika sura ya Nay ili aonekane ni demu.

Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, picha hiyo imeenea huku wengi wakikitafsiri kitendo hicho kuwa ni cha kutaka kumdhalilisha Mbongo Fleva huyo aonekane ni shoga.

Katika wimbo huo ulioleta figisufigisu, kuna kipengele Nay alisema Wema hana mimba bali anatafuta kiki ya msimu hali iliyotibua hasira za Team Wema.

LADY JAYDEE APEWA TARAKA YAKE RASMI

$
0
0

Judith Wambura Mbibo ‘Jide
BAADA ya mvutano wa muda mrefu, hatimaye diva wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ amepewa talaka rasmi kwenye Mahakama ya Manzese, Sinza jijini Dar.

Jide alifungua kesi ya madai ya talaka katika mahakama hiyo baada ya kutofautiana na mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Captain’, aliyekuwa mumewe wa ndoa kabla ya kumwagana takriban miaka miwili iliyopita.

Gardner G. Habash ‘Captain’

Taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika, wawili hao waliooana mwaka 2005, walitinga katika viunga vya mahakama hiyo Alhamisi iliyopita kisha hukumu ya kesi hiyo kusomwa na talaka rasmi kutolewa kwa Jide na Gardner.

“Nimemuona Jide na Gardner hapa, wamekuja kusikiliza hukumu yao. Taarifa za uhakika ni kwamba tayari mahakama imevunja rasmi ndoa na kila mmoja kapewa hati yake ya talaka na sasa kila mtu yupo huru kuendelea na maisha yake,” kilisema chanzo.

Baada ya taarifa hizo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alimtafuta Jide ili aweze kuzungumzia hatua hiyo waliyoifikia lakini simu yake haikuwa hewani kama ilivyokuwa kwa Gardner lakini bahati nzuri mmoja wa ndugu wa mrembo huyo mkongwe wa Bongo Fleva aliyeomba hifadhi ya jina alipatikana na kufunguka:

“Ni kweli tulikuwa mahakamani. Jide ameshapewa talaka yake na kila kitu kimeenda vizuri. Gardner naye kapewa hati yake ya talaka hivyo kuanzia sasa kila mmoja yupo huru kufanya yake.”
Viewing all 110 articles
Browse latest View live