↧
USIKU WA LOVE POTION YA BELL9 & JUX ULIVYOFANA NDANI YA UKUMBI WA SKY NIGHT LIFE MASAKI JIJINI DAR ES SALAAM
↧
ANGALIA JINSI RUBY ALIVYOWAPAGAWISHA MASHABIKI ZAKE NDANI YA MAISHA BASEMENT
![]() |
Meneja matukio wa Maisha Basement Hemedi Kavu 'HK', akiongea jambo kabla ya kuwakabidhi zawadi ya Valentine's Day mashabiki waliojitokeza jukwaani hapo. |
↧
↧
RAIS DKT MAGUFULI AWAPA ULAJI MPYA ROSE MIGIRO,CHIKAWE!
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.
Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.
![]() |
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. |
Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia.
Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni.
Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
15 Februari, 2016
↧
SIMANZI MWANAMUZIKI JOHN WOKA AFARIKI DUNIA!
↧
UKWELI WA TAJIRI ALIYE AUAWA NA MAMACHINGA HUU HAPA!
![]() |
Mchumba wa tajiri huyo kiuaga mwili wa mpendwa wake. |

Mchumba wake akiwa amezimia.
Stori: Makongoro Oging’, Uwazi
DAR ES SALAAM: Inauma sana! Mfanyabiashara mkubwa wa Kariakoo jijini Dar, Stephen Elija Silas (27) ameuawa kwa kupigwa mawe na wafanyabiashara wadogowadogo ‘Wamachinga’ kwa madai ya kukanyaga kwa gari lake nyanya walizopanga barabarani, Uwazi limefuatilia.
Tukio hilo lenye simulizi ya kusikitisha lilijiri usiku saa nne ya Februari 8, mwaka huu katika makutano ya Mtaa wa Msimbazi na Aggrey, Kariakoo jijini Dar es Salaam wakati marehemu huyo alipokuwa akilikwepa gari lililobeba maziwa.
Marehemu Stephen alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T 312 AZU ambalo pia lilipondwa kwa mawe na Wamachinga. Alikuwa njiani kuelekea nyumbani kwake, Kinondoni, Dar.![]()

Marehemu Stephen na mchumba wake.
MBALI NA MAWE, ALICHOMWA KISU
Taarifa zaidi zinadai kuwa, mbali na marehemu huyo kupigwa mawe, pia Wamachinga hao walimchoma kisu kwenye kwapa la mkono wa kulia akiwa ndani ya gari.
SHUHUDA ASIMULIA
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema marehemu alikuwa akitokea upande wa uliyokuwa mzunguko wa Shule ya Uhuru, akaingia Barabara ya Msimbazi. Alipofika makutano ya mtaa huo na Aggrey, mbele yake kulikuwa na gari lililobeba maziwa ambalo liliyumba, hivyo ili asiligonge akalikwepa na hivyo kujikuta akikanyaga kwa bahati mbaya nyanya za Wamachinga hao ambao palepale walianza kumshambulia kwa maneno, baadaye mawe na kumalizia na kisu.![]()

WALICHANGANYIKA NA WAHUNI
“Jitihada za wasamaria wema kumuokoa zilishindikana licha ya jamaa kuomba msaada. Mimi naamini kuwa, mbali na Wamachinga pia wahuni wa mitaani walikuwepo kwa lengo la kupora vitu vyake,” kilisema chanzo hicho.
ALIOMBA MSAMAHA
Chanzo: “Kwanza jamaa alipobaini amekanyaga nyanya za biashara ya Wamachinga hakufanya fujo kwa kunena mabaya, aliomba asamehewe au alipe fedha kulingana na nyanya zilizoharibika lakini Wamachinga na wahuni hao hawakumsikiliza, waliendelea kumwadhibu.
“Kulikuwa na wananchi waliokuwa wakitokwa machozi walipomuona jamaa akipigwa mawe kwa kosa ambalo halina kichwa wala miguu.”
WANANCHI WAPIGA SIMU POLISI
Inaelezwa kuwa, baadhi ya wananchi waliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Msimbazi ili wakamuokoe Stephen lakini licha ya kuwahi katika eneo la tukio, walimkuta akiwa hoi kutokana na kipigo na alifariki dunia wakati polisi wakimkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
UWAZI LAFIKA MSIBANI
Uwazi kama ada yake, lilifika kwenye msiba wa Stephen, kwa baba yake mkubwa marehemu aitwaye Charles Losaru, Mtoni Kijichi jijini Dar na kuzungumza na mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Rebeca Elija ambaye alisema alikuwa na marehemu muda mfupi kabla ya kifo chake. Alikuwa na haya ya kusema:
“Marehemu kaka Stephen alikuwa mfanyabiashara mwenye maduka ya bidhaa mbalimbali, Kariakoo na Sinza. Huwa ana kawaida ya kutusindikiza na gari lake baada ya kufunga maduka. Mimi na ndugu zangu wengine tunaishi Kitunda yeye Kinondoni. Amekuwa akitusindikiza hadi Banana na kutuacha tupande daladala.

“Siku ya tukio, alitusindikiza na kutuacha Buguruni. Ilikuwa saa tatu usiku. Ni sisi tuliamua atuache hapo badala ya Banana. Yeye akarudi akipitia Kariakoo kwa vile kuna ndugu zetu wengine wana maduka maeneo hayo.”
SIMU YAKE YAPIGWA, YAITA TU!
Rebeca anaendelea: “Tuliposhuka kwenye daladala pale Banana, nilimpigia simu mara tatu ikawa inaita bila kupokelewa. Nikampigia simu mchumba wake, anaitwa Neema William ambaye ilikuwa wafunge ndoa hivi karibuni. Nilitaka kujua kama kaka alishafika nyumbani, Neema akasema hajafika.
TAARIFA ZA KIFO KWA NDUGU
“Sasa wakati tunapanda daladala Banana kwenda Kitunda, nilipigiwa simu na marafiki zake na kuniambia kuwa Stephen amepata matatizo yupo Muhimbili. Niliposhuka Kitunda, alinipigia simu kaka yangu mkubwa, anaitwa Silas ambaye tulikuwa naye Kariakoo, akaniambia kaka amefariki dunia (machozi).

MAREHEMU AAGWA DAR, AZIKWA ARUSHA
Mwili wa marehemu Stephen uliagwa Alhamisi ya wiki iliyopita katika Kanisa la Anglikana lililopo Muhimbili na kusafirishwa kwenda nyumbani kwao, Daraja Mbili mkoani Arusha kwa mazishi yaliyofanyika Ijumaa iliyopita.
POLISI WAZUNGUMZIA
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, ACP Ernest Matiku alipohojiwa na Uwazi ofisini kwake wiki iliyopita, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa, marehemu alipigwa na kundi la watu baada ya kugonga gari lililokuwa likiuza maziwa kisha kukanyaga bidhaa za Wamachinga zilizokuwa zimepangwa chini.

“Mpaka sasa tunawashikilia watu kumi kutokana na tukio hilo na bado upelelezi unaendelea. Kwa sasa hakuna biashara ya Wamachinga inayoendelea maeneo yale ya Mtaa wa Msimbazi.
“Nalaani kitendo kile cha mauaji kwani hata kama marehemu alifanya kosa lakini sheria zipo na siyo kuchukua maamuzi hayo mazito ya kukatisha maisha ya binadamu, wote waliofanya unyama ule watashughulikiwa kisheria upelelezi ukikamilika,” alisema kamanda huyo.
↧
↧
ANGALIA JINSI MKE WA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ALIVYOAGA SHULENI KWAKE MBUYUNI!

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni alipowasili katika shule ya Msingi ya Mbuyuni, Oysterbay, jijini Dar es salaam kwa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi ya saa toka kwa mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasiojiweza katika shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Oysterbay, jijini Dar es salaam katika sherehe hiyo fupi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza risala toka kwa mwanafunzi wa shule ya Msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.
↧
SIMBACHAWANE AWAPIGA CHINI WAKURUGENZI WANNE WA HALIMASHAURI!

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne kwa tuhuma za kuwahonga wakaguzi wa fedha kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) ili wapewe hati safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi .
Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera, Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara na Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.
Pia,Waziri Simbachawene amemsimamisha kazi mkurugenzi Halmashauri ya Tunduma Mkoani Mbeya Bi Halima Ajali ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika shuguli za halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato.
Aidha, Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake
Akibainisha makosa ya kila mkurugenzi,Waziri Simbachawene amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu alimwagiza mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa wa ofisi ya CAG kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo huku akijua ni kosa kisheria. Watumishi wa wa ofisi ya CAG waliopokea pesa hizo ni Stevin Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole
Katika Halmashauri ya Nanyumbu, Simbachawene amesema kuwa tarehe 26 Juni 2015, mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa walimkabidhi fedha Milioni 3 na laki tano afisa wa ofisi ya CAG kwa lengo la kutoa hati safi
Waziri Simbachawene amesema mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume na mweka hazina wake waliwapatia milioni 16 maafisa wakaguzi wa ofisi ya CAG ili wafiche ufisadi walioubaini
Amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ikiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi
↧
MICHAEL OLUNGA APATA TIMU ULAYA, NI BAADA YA KUKOSA NAFASI KKATIKA CLUB YA ARSENAL!
![]() |
Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Gori Mahia ya Kenya Michael Olunga. |
Mchezaji wa timu ya Gori Mahia ya Kenya ambaye kwa muda mrefu alikuwa na ndoto za kuchezea timu ya Arsenal ya England, hatimaye ameamua kutimkia nchini Sweden ambako amesaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Djurgardens baada ya kukwama kupatiwa nafasi ya kujiunga na timu ya Arsenal.
Michael Olunga mwenye umri wa miaka 21 mwaka jana mwezi wa 8 alitengeneza video na kumuomba meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ili ampatie nafasi ya kumsajili kutoka kwenye klabu yake ya Gor Mahia ya Kenya lakini ikashindikana na kuamua kubadili gia yake na kutimukia nchini Sweden ambapo amefanikiwa kuingia kadarasi ya miaka minne.
Akizungumza mmoja wa wasimamizi wake alisema kuwa Olunga amekuwa mtu mwenye ndoto za kufika mbali kisoka hivyo kila kukicha amekuwa akijituma kadri ya uwezo wake na kwa namna hiyo siku moja atakuja kutimiza ndoto zake za kuichezea hata klabu ya Arsenal.
“Anajitahidi sana, anajifunza kwa malengo mara zote anataka kujifunza ili kupiga hatua”, Mkurugenzi wa michezo Bosse Andersson alisema.
“Kwa maendeleo na mazingira yetu rafiki na yenye utulivu ya Djurgardens atajifunza na atakuwa bonge la Straika atakayeweza kucheza katika ligi kubwa Ulaya.
Hayo ndiyo matarajio ya Michael na anayosifa ya kufanya hivyo.
Olunga ambaye jina lake la utanini ‘Engineer’ kwa maana mhandisi kutokana na kuwa na Degree ya Uhandisi amesema anatambua kuwa itakuwa vigumu kuzoea mazingira haraka.
“Mwanzoni itabidi nijaribu kwenda lakini nikishazoea basi nitaendelea kufunga zaidi na zaidi. Aliiambiatovutiyaklabuhiyo”.
“Mpaka sasa nimeshacheza mechi za kirafiki tu lakini najiona ni povizuri”.
“Kila kitu kimeandaliwa vizuri uwanja wa kufanyia mazoezi upo safi, unaonekana kama upotayari kwakuchezea ligi kubwabarani Ulaya”.
↧
WAGANDA KUMCHAGUA RAIS WAO MPYA LEO!

Wagombea wanane wanachuana kuwani kiti cha Rais.
Wananchi wa Uganda waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kumchagua Rais na wawakilishi wao wa Bunge.
Inaelezwa kuwa, raia wapatao milioni 15 wa nchi hiyo waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanamchagua Rais mpya wa nchi hiyo pamoja na wawakilishi wao wa Bunge lijalo. Wagombea wanane wanachuana kuwani kiti cha Rais. Hata hivyo kati ya wagombea hao wanane ni watatu tu miongoni mwao ndio waliotajwa sana katika kampeni za uchaguzi huo.
Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani nchini Uganda tangu mwaka 1986 anachuana na Kizza Besigye mgombea wa chama cha FDC na Amama Mbabazi aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wake. Uchaguzi wa leo unafanyika huku wapihzani wakiendelea kulalamika kwamba, serikali ya Rais Museveni imekuwa ikiwabana na kuwakandamiza wafuasi wao hasa katika kampeni za uchaguzi wa mara hii. Huku Tume ya Uchaguzi ya Uganda ikisisitiza kwamba, uchaguzi wa leo utakuwa huru na wa haki, wagombea wa upinzani wameonya kuhusiana na hatua yoyote ile ya kuiba kura au kufanya udanganyifu.
Amama Mbabazi amesema, hatayakubali matokeo ya uchaguzi huo endapo itabainika kwamba, kulikuwa na mchezo mchafu wa kuiba kura. Weledi wa mambo wanasema, kuna uwezekano mkubwa Rais Museveni akashinda tea kiti cha urais na kuendelea kutawala nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
↧
↧
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA RAIS DKT. JOHN P. MAGUFULI AKIONGEA NA WASANII IKULU!


Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.![]()


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.





Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na kundi la sanaa la Tanzania One Theatre baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016,
Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wataalamu wa TEHAMA baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Fleva baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.






Rais John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye kabla ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.

Rais John Pombe Magufuli na Mkewe, Mama Janeth Magufuli wakiongozana na Mhe January Makamba huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye wakielekea ukumbini kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.

Rais John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mhe January Makamba huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye kabla ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
PICHA NA IKULU
↧
ANGALIA PICHA KADHAA ZA MATUKIO YA SHAMSA FORD NA KIVAZI CHAKE!
↧
HAYA NDIYO MATUKIO KATIKA PICHA MPYA ZA SHILOLE NA BWANA AKE MPYAAAA
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu juzikati jioni alitinga nyumbani kwa Shilole na kufanikiwa kuwakuta wawili hao lakini katika hali ya kushangaza, baada ya kuona kamera wakaanza kufanyiana vituko vya kimahaba.
![]() |
Shilole na Medy Music wakiperuzi kitu kwenye simu huku furaha ikitawala. |
Shilole alionekana kumshikashika Medy huku dogo huyo aliyeonekana kuwa kama kalewa akitoa ushirikiano.Katika meza iliyokuwepo sebuleni kulikuwa na chupa za bia lakini mara kadhaa Shilole alionekana akinywa juisi huku dogo akipiga maji, mazingira yaliyoonekana kuwa Shilole alikuwa akimlewesha kwa makusudi kisha mambo ya ‘kuchi…kuchi’ yachukue nafasi.
![]() |
Shilole na Medy Music hapa sijui wamegundua jambo gani la kushangaza. |
Akizungumzia uhusiano wake na Medy, Shilole alikiri kuwa ndiye mpenzi wake kwa sasa na akawataka wanaodai anambemenda wakidhani ni mtoto wakae kimya.“Huyu ndiye laazizi wangu kwa sasa, ana kila sifa ya kuwa mume wangu na wala siyo mtoto, ni mtu mzima kabisa tofauti na Nuh,” alisema Shilole kisha kuendelea kumdekea jamaa huyo aliyeonekana kafa-kaoza kwa staa huyo.
Wakati Shilole akifanya yake, Nuh naye juzikati alitupia picha kadhaa mtandaoni akiwa kimahaba na demu mkali aliyefahamika kwa jina la Erah Erah anayedaiwa kuwa mpenzi wake.
![]() |
Mhaba mapya kati ya Shilole na Medy Music. |
↧
RAY: NAY WA MITEGO HANA NIDHAMU YA KUHESHIM WAKUBWA!
![]() |
Staa wa filamu Tanzania Vicent Kigos 'Ray'. |
STAA wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa mara nyingine ameendelea kuteka ‘headlines’ baada ya kuibuka na kudai kuwa alishawahi kumuokoa staa wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego asipigwe.
Akizungumza asubuhi hii katika kipindi cha Leo Tena kinachorusha na Clouds FM, Ray alisema kuwa alipokuwa katika shoo ya Fiesta Mwanza, Nay alivamiwa na kundi la wasanii wa Bongo Movie na kutaka kupigwa.
“Nilifanikiwa kumzuia kwasababu wasanii walikuwa wengi wakiongozwa na Wema Sepetu sasa nashangaa mwenzangu Nay ananisakama natumia pesa zote za mauzo ya filamu namalizia kwenye mkorogo,” alisema Nay.
![]() |
Ray akiwa katika mazoezi yake ya kila siku. |
↧
↧
MZIMU WA OSTAZ JUMA NAMUSOMA WAZIDI KUWATESA WASANII HAWA!!
Miongoni mwa mameneja Tanzania waliosaidia kuusimamisha muziki wa Bongo Fleva na Dansi, Ostaz Juma Namusoma. |
UKIZUNGUMZIA miongoni mwa wadau wakubwa wa muziki waliosaidia kuusimamisha muziki wa Bongo Fleva na Dansi nchini ni wazi jina la Ostaz Juma Namusoma litakuwa miongoni mwa majina utakayoyataja.
Kabla ya kuwasimamia wanamuziki wa Bongo Fleva, Ostaz Juma Namusoma alikuwa akiwasaidia sana wanamuziki wa Dansi kama vile Ali Chocky, Super Nyamwela, Jose Mara, Kalala Junior, Nyoshi El-Saadat, Christian Bella, Mwinjuma Muumini na wengine wengi.
Ikumbukwe kuwa hata Wimbo wa Ubinadamu ulioimbwa na Christian Bella ulikuwa maalum kwa mdau huyo wa muziki. Ostaz Juma aliamua kuupa kisogo muziki wa Dansi na kujikita kwenye Bongo Fleva ambapo alianzisha Kampuni ya Watanashati iliyokuwa na vichwa kama vile, PNC, Marehemu Sharomilionea,Kitale, Suma Mnazareti pamoja na Dogo Janja.
Wasanii hao wote kwa sasa hawapo chini yake kutokana na kila mmoja kuondoka kwenye kampuni hiyo na huku nyuma yake akimwagia maneno mbofumbofu na kejeli nyingi kwa mdau huyo na baada ya muda tangu watoke walijikuta wakishindwa kuendana na soko la muziki.
Katika makala haya yanawachambua wasanii hao ambao mzimu wa Ostaz Juma bado unazidi kuwatesa.
![]() |
Msanii wa Bongo Fleva aliyewahi kuwa chini ya usimamizi wa Ostaz Juma Namusoma kupitia kampuni ya Mtanashati PNC akiwa katika pozi. |
PNC
Pancras Ndaki kama anavyojulikana kwenye cheti chake cha kuzaliwa, anaingia kwenye listi ya wasanii waliopitia kwenye mikono ya Ostaz Juma na kupata kusikika vilivyo.
PNC alikaa na Ostaz Juma kwa muda mrefu na kuamua kujitoa huku sababu akiitaja ni mambo kumwendea mrama kwa kuwa alikuwa akijaribu kutoa nyimbo za kila aina kulishawishi soko gumu la muziki wa Bongo Fleva lakini mambo hayakuwa sawa.
Aliamua achukue uamuzi mgumu wa kujiondoa na kuanzisha kundi la Top Fleva huku akidai alikuwa hapati msaada wowote kwa bosi wao (Ostaz Juma) na kwamba anawasema vibaya kwenye media. Baada ya kusema hayo tu miezi michache, PNC alirudi na kumpigia magoti Ostaz Juma kumuomba msamaha na kwamba amrudishe kundini.
Msanii aliyekuwa chini ya usimamaizi wa Ostaz Juma Namusoma kupitia kampuni ya Mtanashati Suma Mnazareti katika pozi. |
Suma Mnazareti
Suma Mnazareti naye ni miongoni mwa wasanii wanaoendelea kuandamwa na mzimu wa Ostaz Juma baada ya kujitoa.
Kwa mujibu wa Suma, aliamua kujitoa kwa sababu alikuwa akikosa kile alichokuwa akitarajia na pia aliona kama Ostaz anawajali sana wasanii wa muziki wa Dansi japokuwa alikuwa amejikita kwenye Bongo Fleva.
Baada ya kujitoa kwake alifanikiwa kutoa wimbo na Ommy Dimpoz uitwao Chukua Time ukafanya poa sana kisha Tuko Wangapi akiwa na Tunda Man nao ukafanya poa huku akitoa vijembe kwa Ostaz Juma.
Baada ya hapo, mzimu wa Ostaz Juma ukaanza kumtesa na kujikuta akishindwa kurejea kwenye soko la muziki na kila kazi aliyokuwa akiitoa ilikuwa ikibuma hadi sasa.
![]() |
Dogo Janja. |
Dogo Janja
Abdulaziz Abubakari ama Dogo Janja kwa jina la kisanii, alichukuliwa na Ostaz Juma baada ya kuachana na kundi la Tip Top ambapo alijiunga na wenzake ambao ni PNC pamoja na Suma Mnazareti na kufanikiwa kutoka na wimbo wa pamoja ulioitwa Watanashati.
Baada ya kukaa kwa kipindi kirefu, Dogo Janja alitimuliwa na Ostaz Juma kwa sababu iliyoelezwa ni kukosa heshima na pia kukimbiwa japokuwa alimtafutia shule ambayo alishindwa kusoma.
Dogo Janja aliamua kurudi Tip Top chini ya Madee lakini napo mzimu wa Ostaz Juma uliendelea kumtesa ambapo inaelezwa kuwa hadi sasa ameingia katika mtafaruko mkubwa baada ya kudai kuwa ana kazi zaidi ya 10 ambazo anabaniwa kuzitoa huku akirandaranda mitaani pasipo ishu yoyote.
Ostaz Juma Namusoma katika pozi. |
Msikie Ostaz Juma
Over The Weekend ilifanikiwa kuzungumza na Ostaz Juma juu ya wasanii hao ambapo alifunguka;
“Ujue sisi wadau wa muziki huwa tunaandamwa sana na maneno hasa pale unapoachana na msanii uliyekuwa ukimsaidia. Nimewahi kuwasaidia wasanii wengi kwa mfano ukiangalia mimi na Fella (Said Fella) tunawasimamia wasanii kwa pesa zetu za mfukoni tofauti na mameneja wengine ambao wamekuwa wanasimamia wasanii kwa manufaa yao kama hawapati basi wanaachana na wewe.
“Wasanii hao (Suma, PNC na Dogo Janja) nawatambua kama wasanii waliopitia kwenye mikono yangu, japokuwa kila mmoja aliamua kuondoka lakini naendelea kuwasaida pale wanapokwama hadi leo.
Kweli juzikati nilibahatika kuwa miongoni mwa watanzania wengi niliyesikiliza sauti ya Dogo Janja akiongea na msaichana mmoja huku akitoa lawama kubwa kwa wasimamizi wake wa sasa ambao wamekuwa naye kwa muda mrefu sasa tangu atoke kwangu.
Record hiyo kweli imenisikitisha sana baada ya kumuona kijana wangu akilalama kiasi hicho lakini kikubwa nilichokigundua hapo ni kwamba, mameneja wengi wa wasanii wetu ni tatizo maana wamekuwa wakiwachukua wasanii ili wao wanufaike badala ya kuwasaidia kama nilivyokuwa nikifanya mimi na Said fella.
Kusema kweli kwa haya maneno ya Dogo Janja naanza kuona wazi kabisa kuwa Babu Tale na Madee hawana uwezo wa kummeneji msanii hasa asiyekuwa na fedha maana wao wanataka pesa kutoka kwake huku msanii mwenyewe amekuwa akihitaji msaada wa kikazi na fedha.
Boss wa Mtanashati Ostaz Juma Namusoma katika pozi. |
Mimi suala la mzimu wangu kuwasumbua kweli nimekuwa nikiambiwa na wengi hata baadhi ya wasanii hawa kama PNC juzi kati aliwajhi kuniambia kitu kama hicho, tena akisema kweli mkono wangu si wakuacha vibaya kwani karibia wote niliowahi kuwasimamia wameshindwa kuendelea nje ya Mtanashati na zaidi wanmebaki wakitabika kama unavyomuona Dogo Janja leo hii.
PNC alikuwa akiniambia kuwa kwenye maisha jhakuna mtu asiyekuwa na mapungufu ila mimi kwake nitabaki kuwa kama lulu ya mafanikio kwani pamoja na yeye kutoka kwangu kwa mwembwe nyingi bado amekuwa akinihitaji kwa asilimia kubwa sambamba na wengine wote akiwemo Dogo Janja ambaye ninamsaidia anapokwama,” alisema Ostaz Juma.
Ostaz Juma Namusoma. |
↧
GARDNER: SIMU NDIYO CHANZO CHA NDOA YANGU KUVUNJIKA!
Katika mahojiano maalum yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Gardner alisema hata hivyo, licha ya kutengana kwao, yeye hana chuki na mwanamke huyo aliyeishi naye takriban miaka kumi mfululizo.
Yafuatayo ni mahojiano kamili:
RISASI: Kuna uhusiano gani kati yako na Jide (Lady Jaydee) baada ya kutengana?
GARDNER: Hakuna tunapokutana wala hatuna mawasiliano, kwa hiyo hatuna uhusiano japo mimi sina tatizo lolote wala uadui na yeye, hata hivyo sitashangaa yeye kuonyesha uadui maana ilivyotokea hivyo miezi kadhaa iliyopita.
RISASI: Miezi kadhaa iliyopita kilitokea nini unachotafsiri kama uadui?
GARDNER: Niliona dalili ya chuki wakati fulani nilimshauri tutoe tamko la pamoja kuhusu kutengana kwetu, sababu watu walikuwa wanatuuliza maana hawakutuona pamoja, hakukubali na akataka niwe nasema tu siyo kweli ni uzushi, tuko pamoja japo hatukuwa pamoja hivyo kwa ujinga wangu nilikubali na ndiyo maana nilikuwa najibu watu kuwa sio kweli.
Sasa siku niliyoshtuka ni kwamba mimi nilikuwa nazifuata akaunti zake za mitandao kama mtu niliyekuwa nasimamia kazi zake na niliendelea hivyo miezi kadhaa baada ya kutengana, kwanza nikaambiwa ameenda redioni kutangaza kuwa ameniacha huku mimi ameniambia niseme tu kuwa siyo kweli, ikawa aibu kwangu.
Halafu baadaye nikaona katika mtandao wake kaongea vitu ambavyo aliweka kama anajibu maswali aliyoruhusu aulizwe, lakini kwangu mimi ilikua shambulio, ndipo nilipotafsiri kuna chuki lakini mimi sitamchukia wala siyo adui yake. Kwa sasa ninashukuru talaka imepatikana na najua huu sio mwisho wa kupenda.
RISASI: Hivi ni nini hasa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yenu?
GARDNER: Chanzo anaweza kukisema yeye aliyekataa kuendelea na ndoa, mimi sikuwa na tatizo na yeye, ijapokuwa kutofautiana kwa hapa na pale katika ndoa ni jambo la kawaida, lakini sijajua hadi leo kipi kipya kizito kilifanya yeye atake kutengana.
RISASI: Kwani ilikuwajekuwaje sasa?
GARDNER: Nakumbuka ilikuwa Julai 2014, nilipata booking ya show yake aende kuimba Marekani, ilikuwa ni safari ambayo ingedumu kwa siku saba, lakini mimi nikamshauri akae mwezi mzima yaani aongeze wiki tatu zaidi baada ya show ili iwe ni likizo yake. Basi ilipofika wiki ya tatu ya mwezi huo, ndiyo akanipigia kuniambia akirudi hataki tena kuendelea kuwa katika ndoa.
RISASI: Ulijisikiaje baada ya kupata ujumbe huo?
GARDNER: Kibinadamu mtu umekaa naye miaka mingi ghafla akiwa safarini anakutaarifu kuwa hataki muwe wote tena wakati kaondoka mko sawa, na jana yake mmeendelea kuweka mipango ya maendeleo, nilijisikia vibaya na nilijaribu kutafuta maongezi, alikataa na hakurudi tena nyumbani, ikabidi kukubali ingawa kishingo upande. Nashukuru Mungu nikaanza upya nikaona maisha mapya.
RISASI: Unaweza kusema wakati unakutana na Jide ulimkuta akiwa na nini na wakati mnaachana ulimuacha na nini?
GARDNER: Si uungwana mimi kutangaza nilimkuta na nini labda aseme yeye, lakini tulizalisha mali za kutosha, tulikuwa na vyanzo kadhaa vya fedha na kwa bahati nzuri wewe ulikuwa karibu nasi uliona na wengi waliokuwa jirani nasi wanajua. Mimi nimelelewa kushirikiana na kushea na kamwe siyo kunyang’anyana, ndiyo maana sitasema mambo ya mali, kama kipo ninachostahili nt’akipata tu.
Ijapokuwa yeye amekuwa akipotosha watu kuwa mimi sikuwa na kitu, sikuwa na mchango wa kipato wala wa taaluma katika muda tuliokaa pamoja yaani ni kama Mario ninayemtumia na nilisikitika zaidi pale mahakamani Sinza hakimu alipomuuliza, ninanukuu ‘Kuna mali zozote mlipata wakati mko pamoja katika ndoa,? Yeye akajibu hamna. Hata hivyo mimi sijawahi kuonesha hata nia ya kutaka tugombee mali, nilimpa yeye aamue kila kitu ili kuepuka kulumbana lakini baadaye nikalipuliwa, hahahaha, najua mengi yatasemwa nipakwe ubaya.
Baada ya mahojiano hayo mafupi, gazeti hili lilimtafuta Jaydee na kufanikiwa kumpata kupitia simu yake ya mkononi.
RISASI: Mambo sista?
JAYDEE: Poa, nambie
RISASI: Mashabiki wa kapo yenu wangependa kujua nini hasa kilitokea katika ndoa yenu.
JAYDEE: Hivi stori moja mnaandika mwaka mzima? Kuna kipya gani hapo ambacho hamjaandika? Halafu kulikuwa na mashabiki wa Jaydee, hakukuwa na mashabiki wa couple.
JAYDEE: Hebu kuwa positive, kuna vitu vingi vizuri vya kuandika kuhusu mimi.
↧
KESSY APIGIWA SIMU ZA VITISHO NA BAADHI YA WADAU WA SIMBA KISA MECHI YA WATANI!
![]() |
Beki wa kulia wa timu ya Simba, Hassan Kessy |
BEKI wa pembeni wa Simba, Hassan Kessy, wikiendi iliyopita aliimaliza vibaya baada ya kupokea simu nyingi za mikwara na vitisho akilaumiwa kutokana na kuifungisha timu hiyo ilipovaana na Yanga.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0, beki huyo alisababisha bao la kwanza dhidi ya timu yake, baada ya kumrudishia pasi fupi kipa wake, Muivory Coast, Vincent Angban ambayo ilinaswa na Donald Ngoma na kufunga katika dakika ya 39.
Kosa hilo, lilionekana kuwakera mashabiki wa Simba waliokuwepo uwanjani hapo na kumtolea lawama beki huyo ambaye alikuwa ameonyesha kiwango kizuri kwenye michezo saba iliyopita.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kessy alisema kuwa tangu mechi hiyo ya Yanga imalizike, anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa mashabiki ambao kila wakati wanampigia simu na kumtumia meseji za mikwara na vitisho.
Kessy alisema, anashangaa kuona mashabiki hao wakiendelea kumpigia simu na kumtumia meseji, licha ya kuwaomba msamaha kwa makosa hayo aliyoyafanya.
Aliongeza kuwa, kikubwa anachokifanya yeye hivi sasa ni kukaa kimya ili kuepusha matatizo mengine kwa faida yake na badala yake anaendelea kutimiza majukumu yake ya ndani ya uwanja akiwa na Simba.
“Mchezo wa soka ni wa uvumilivu sana na hadi hapa nilipofikia kukaa kimya kugombana na shabiki yeyote nimejitahidi kutokana na simu ninazopigiwa na meseji ninazotumiwa na mashabiki wa Simba.
“Wengi wao wanaonipigia simu na kunitumia meseji, wanalalamika kuwa mimi nimesababisha tufungwe baada ya kufanya kosa la kurudisha pasi fupi kwa kipa kabla ya Ngoma kufunga.
“Kikubwa wanachotakiwa kukifahamu ni kuwa, soka ni mchezo wa makosa ambayo mimi niliyafanya na kusababisha tufungwe bao moja katika kipindi cha kwanza, ninaomba nichukue nafasi hii kuwaomba radhi Wanasimba wote,” alisema Kessy.
Aidha, alipotafutwa meneja wa mchezaji wa timu hiyo, Athumani Tippo kuzungumzia suala hilo, kwanza kabisa alikiri kuwepo na taarifa hizo za mchezaji wake kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba.
“Hizo taarifa za kweli kabisa, mchezaji wangu wanamtumia meseji na kumpigia simu za vitisho, hivyo hivi sasa nimepanga kukutana na mwanasheria wangu ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake,” alisema Tippo.
↧
SKY LIGHT BAND YAWAPAGAWISHA MASHABIKI ZAKE NDANI YA MAISHA BASEMENT
![]() |
Badhi ya mashabiki wa Sky Light Band wakicheza kwa staili ya pamoja ndani ya ukumbi wa Maisha Basement. |
USIKUwa kuamkia leo Sky Light Band iliendeleza kutoa burudani zake ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo mashabiki kibao walihudhuria na kujumuika kwa pamoja kupata muziki muzuri uliokuwa ukipigwa na bendi hiyo.
![]() |
Waimbaji wa Sky Light Band wakiwapagawisha baadhi ya mashabiki zao waliojitokeza kufuatilia burudani zao ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement Kijitonyama jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. |
![]() |
Muimbaji wa Bendi hiyo Sone Massamba (katikati), akiongoza burudani hizo huku mmoja wa mashabiki zake akionyesha hali ya kupagawishwa na sauti yake. |
![]() |
Waimbaji wa Sky Light Band wakiimba kwa hisia kali. |
![]() |
Badhi ya mashabiki wa bendi hiyo wakicheza kwa staili ya pamoja. |
![]() |
Sone Massamba akiwaonyesha mashabiki zake staili ya kucheza mmoja ya wimbo wa bendi hiyo. |
![]() |
Mashabiki wakijaribu kuiga staili walizoonyeshwa. |
![]() |
…Wakionyesha uelewa wao baada ya kufundishwa kucheza. |
↧
↧
MAZISHI YA MZEE MAPILI KUFANYIKA KISUTU LEO!
↧
INFANTINO NDIYE RAIS MPYA WA FIFA

Rais mpya wa FIFA, Gianni Infantino ametoa ahadi ya kufanya kazi na wote na kurudisha heshima ya FIFA.

Matokeo ya raundi ya kwanza.

Sheikh Salman al-Khalifa (kulia) akiwa na Gianni Infantino (wa katikati) walioingia round ya pili.
Infantino ameibuka na ushindi wa kura 115 dhidi ya Sheikh Salman aliyepata 88.
↧
JOKATE,KIBA WADAIWA KUZICHAPA MCHANA KWEUPEEEE!

Wapendanao, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Kiba ‘King Kiba’ wakiwa katika pozi.
Na mwandishi wetu, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Wapendanao, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Kiba ‘King Kiba’, wamedaiwa kuzichapa kavukavu ndani ya gari kisa kikiwa ni ujumbe mfupi wa maneno (SMS), Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilitokea katikati ya wiki iliyopita maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam bila kujulikana walikuwa wakitokea wapi kwenda wapi.

Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Jokate na Kiba awali walimwagana lakini hivi karibuni wakarudiana baada ya familia ya Kiba, akiwemo mama yake, kuwakutanisha Februari 5, mwaka huu kwenye Hoteli ya Slipway, Masaki jijini Dar na kumaliza tofauti zao.
Siku hiyo ya kupatanishwa kulikuwa na hafla ya uzinduzi wa video ya Kiba iitwayo Lupela ambayo inafanya vizuri katika soko la muziki wa Bongo Fleva nchini.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Jokate na Kiba walipishana kauli baada ya mrembo huyo anayefanya vyema katika tasnia ya muziki, filamu na mitindo Bongo kulazimisha kusoma ujumbe mfupi wa maneno ulioingia kwenye simu ya mpenzi wake huyo.

Ali Kiba ‘King Kiba’.
SIKU YA TUKIO
Chanzo hicho kiliweka bayana kuwa wawili hao wakiwa katika mizunguko yao hivi karibuni, walisimamisha gari lao maeneo ya Kinondoni-Biafra na ndipo walipoanza kuzozana kwa muda kabla ya kuanza kushikana maungoni.
“Walitaitiana kwenye gari. Wakapaki, Kiba alionekana kushuka kama anataka kumuacha Jokate peke yake ndani ya gari, Jokate hakukubali, akashuka na yeye kumlazimisha arudi. Mazungumzo yalisikika Jokate akihoji ni kwa nini jamaa anamkatalia kusoma meseji iliyoingia kwenye simu yake! Ndipo timbwili liliponoga.
“Ilikuwa mtiti wa aina yake lakini Kiba alipoona ‘nzi’ (mashuhuda) wanaanza kujaa, akaona isiwe tabu, akarudi ndani ya gari na Jokate naye akaingia wakaondoka zao,” kilisema chanzo hicho kilichoshuhudia timbwili zima.
MENEJA AFUNGUKA
Kabla ya kuwatafuta wawili hao, mwanahabari wetu alimtafuta mmoja kati ya mameneja wa Kiba aliyeomba hifadhi ya jina ambaye aliweka wazi kuwa, wawili hao walipishana ‘Kiswahili’ kutokana na SMS ambayo haikuwa mbaya isipokuwa walishindwa kudhibiti hasira zao.
Msikie: “Walipishana lugha baada ya Jokate kulazimisha kusoma au kuona ujumbe ulioingia kwenye simu ya Kiba. Halafu kwani unafikiri basi ulikuwa ujumbe mbaya, ilikuwa ni meseji yangu niliyomtumia kumpa maelekezo ya kazi lakini Jokate akamaindi.
“Alichokosea Kiba ni kukataa kumpa simu sasa sijui naye ana vimeo vyake au vipi lakini hapo ndipo utata ulipoanzia. Wakavutana kwa muda lakini bahati nzuri Kiba akawa mstaarabu, akarudi ndani ya gari kama Jokate alivyomtaka, wakamalizana na kuendelea na safari yao,” alisema meneja huyo.
PENZI LIPO PALEPALE
Akaongeza: “Kwa sasa wapo freshi. Si unajua mambo kama hayo kwenye mapenzi yanatokea. Wamewekana sawa na kila kitu kipo kwenye mstari. Wamewekeana mikakati mizuri kuhusu matumizi ya simu.”
KIBA ANASEMAJE?
Baada ya kuzungumza na meneja huyo, mwanahabari wetu alimtafuta King Kiba kupitia kilongalonga chake cha mkononi ambapo alipopatikana alitoa majibu tata ambayo gazeti lilishindwa kubaini kama amekubali au amekataa.
Msikilize: “Kwa nini kila siku mnaniuliza habari za skendo tu? Mbona hamniulizi kuhusu muziki wangu unavyofanya vizuri kitaa au hujasikia ngoma yangu ya Lupela inavyokamata chati? Acha mambo yako bwana.”
Akaongeza: “Halafu, hata kama ni kweli wewe tatizo lako ni nini? Mengine ni mambo binafsi. Haipendezi kila ninachofanya au kinachonitokea nikitangaze kwenye vyombo vya habari. Mimi nafikiri uwe unaniuliza zaidi kuhusu kazi yangu ambayo mashabiki ndiyo wanataka kuijua.” (akakata simu).
JOKATE HAPOKEI SIMU
Jitahada za kumpata Jokate ili aweze kuzungumzia sakata hilo ziligonga mwamba baada ya mrembo huyo kutopokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu chochote.
Jokate na Kiba kwa sasa ni ‘kapo hot’ ambayo mashabiki wengi wanawaombea wafikie hatua ya kuoana licha ya kuwa na mvutano kutoka kwa wazazi wa Jokate ambao waliwahi kuripotiwa kutoafiki uhusiano huo.
↧